Shamba
 la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa 
baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini 
mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya 
Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili 
makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi 
hiyo.
Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa 
akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara iliyopatikana ni zaidi ya 
shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya 
Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadahara
 kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi watumie nguvu ya umma 
kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.Kamanda wa 
polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata 
hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya 
uharibifu huo mkubwa namsako unaendelea kuwatafuta wengine waliohusika 
katika tukio hilo.

No comments:
Post a Comment