MOURINHO: KUMLINGANISHA RONALDO NA MESSI SASA NI MARUFUKU
KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho 
amewasifu Cristiano Ronaldo na nyota wa Barcelona, Lionel Messi baada ya
 wawili hao kufunga mara mbili kila mmoja katika sare ya 2-2 juzi usiku 
na ametaka ipigwe marufuku kuwalinganisha. 
Alipoulizwa nani anapaswa kutwaa tuzo ya Ballon d'Or ya mwanasoka bora wa dunia, alisema: "Sitaki kuiwaza sana hiyo. 
"Nadhani ipigwe marufuku sasa kusema nani ni mwanasoka bora wa dunia kwa sababu hawa wawili ni wa sayari nyingine. 
"Ningependa mchezaji wangu ashinde kwa 
sababu yeye ni bingwa wa ligi bora duniani, lakini nadhani wote ni 
wachezaji wazuri sana."


No comments:
Post a Comment