MAJINA YA WANOWANIA TUZO ZA MCHEZAJI BORA AFRICA HAWA HAPA!!!
CAIRO, Misri
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF)
limetaja majina ya awali ya wachezaji nyota 34 barani wanaowania tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Afrika Mwaka 2012 ambamo ndani yake, wamejaa 'maproo'
29 wanaocheza soka la kulipwa nje ya Afrika huku nyota wa TP Mazembe,
Mtanzania Mbwana Samatta na Tressor Mputu wanaong'ara katika Ligi ya
Klabu Bingwa Afrika wakikosekana kwenye orodha hiyo.
Miongoni mwa wanaocheza soka la kulipwa
Ulaya ni mshindi wa tuzo hiyo msimu uliopita, kiungo wa timu ya taifa ya
Ivory Coast na klabu ya Manchester City ya England, Yaya Toure,
mastraika nyota wa Newcastle United -- Papiss Demba Cisse na Demba Ba na
pia winga wa Arsenal, Gervinho..
Wachezaji watatu wanaocheza katika klabu
za Afrika ni Wazambia Rainford Kalaba na Stoppila Sunzu wanaoichezea TP
Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Youssef Msakni wa
Esperance ya Tunisia.
OROTHA KAMILI:
1. Abdelaziz Barrada - Getafe (Hispania) na Morocco
2. Adel Taarabt - Queens Park Rangers (England) na Morocco
3. Alain Sibiri Traore - Lorient (Ufaransa) na Burkina Faso
4. Alexander Song - Barcelona (Hispania) na Cameroon
5. Andre 'Dede' Ayew - Marseille (Ufaransa) na Ghana
6. Arouna Kone - Wigan (England) na Ivory Coast
7. Aymen Abdennour - Toulouse (Ufaransa) na Tunisia
8. Bakaye Traore - AC Milan (Italia) na Mali
9. Cheick Tiote - Newcastle United (England) na Ivory Coast
10. Christopher Katongo - Henan Construction (China) na Zambia
11. Demba Ba - Newcastle United (England) na Senegal
12. Didier Drogba - Shanghai Shenhua (China) na Ivory Coast
13. Emmanuel Agyemang-Badu - Udinese (Italia) na Ghana
14. Emmanuel Mayuka - Southampton (England) na Zambia
15. Foxi Kethevoama - FC Astana (Kazakhstan) na Afrika ya Kati.
16. Gervinho - Arsenal (England) na Ivory Coast
17. Hilaire Momi - Le Mans (Ufaransa) na Afrika ya Kati.
18. John Obi Mikel - Chelsea (England) na Nigeria
19. John Utaka - Montpellier (Ufaransa) na Nigeria
20. Kwadwo Asamoah - Juventus (Italia) na Ghana
21. Moussa Sow - Fenerbahce (Uturuki) na Senegal
22. Nicolas N'koulou - Marseille (Ufaransa) na Cameroon
23. Papiss Demba Cisse - Newcastle United (England) na Senegal
24. Pape Moussa Konate - FC Krasnodar (Urusi) na Senegal
25. Pierre-Emerick Aubameyang - St Etienne (Ufaransa) na Gabon
26. Rainford Kalaba - TP Mazembe (DR Congo) na Zambia
27. Seydou Doumbia - CSKA Moscow (Urusi) na Ivory Coast
28. Seydou Keita - Dalian Aerbin (China) na Mali
29. Sofiane Feghouli - Valencia (Hispania) na Algeria
30. Stoppila Sunzu - TP Mazembe (DR Congo) na Zambia
31. Victor Moses - Chelsea (England) na Nigeria
32. Yaya Toure - Manchester City (England) na Ivory Coast
33. Younes Belhanda - Montpellier (Ufaransa) na Morocco
34. Youssef Msakni - Esperance (Tunisia) na Tunisia
No comments:
Post a Comment