Thursday, November 1, 2012

KESI YA PONDA: MAMBO YALIVYOKUWA, ULINZI HAIJAWAHI KUTOKEA

Sheikh Ponda Issa Ponda, akifunguliwa pingu, baada ya kufikishwa kwenye chumba cha mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana Alhamisi Novemba 1, 2012. Kiongozi huyo mwenye msimamo mkali, alifikishwa kwa mara ya pili jana pamoja na wafuasi wake ambapo hakimu anayesikiliza kesi dhidi yake, Victoria Nongwa, ya kuvamia eneo la Markaz, Chang'ombe jijini Dar es Salaam, ambapo waliharibu  na kuiba mali vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni 59, madai ambayo washtakiwa wote waliyakanusha. Hakimu huyo alikubali kutoa dhamana kwa washtakiwa wote isipokuwa kiongozi huyo ambaye ni mshtakiwa namba 1 kwa madai kuwa bado Mkurugenzi was Mashtaka nchini (DPP), hajaondoa pingamizi lake la kuzuia dhamana kwa mshtakiwa namba moja. Ulinzi katika mahakama hiyo haujawahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine, palifungwa CCTV Cameras, vifaa vya kugundua vitu vyenye asili ya chuma, polisi wa kutuliza gharsia magereza na wale wa FFU, polisi wa farasi na mbwa, pamoja na askari kanzu waliotapakaa kila kona ya maeneo jirani na mahakama hiyo kubwa jijini Dar es Salaam. Kikundi kidogo cha wafuasi wa ssheikh Ponda, kilijaribu kuleta rabsha, lakini polisi walitumia busara na kuwaelekeza kilichoamuliwa mahakamani ambapo pamoja na kusuasua kuondoka eneo hilo la mahakama, lakini hatimaye waliondoka huku  polisi wa kutuliza ghasia wakiwafuata kwa nyuma hadi eneo la makutano ya barabara za Bibi Titi na ile ya Morogoro nao wakatawanyika. Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika vya habari, kulikuwepo taarifa kuwa wafuasi hao walipanga kutega milipuko kwenye eneo la mahakama na pia walisambaza vipeperushi vyenye vitisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufanbya maandamano makubwa ya kulazimisha kiongozi huyo aachiliwe. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Novemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena
Wafuasi wa Ponda, wanbaoshatakiwa pamoja naye, wakifunguliwa pingu mahakamani
Mshtakiwa akiwa amebebwa na mwenzake baada ya kudondoka mahakamani na kupoteza fahamu

 

 

 

Huiingii mahakama ya Kisutu bila ya kukagulkiwa na mashine za kugundua vitu vya asili ya chuma hapo jana Alhamisi Novemba 1, 2012
Farasi wa polisi wakiwafukuza wafuasi wachache wa Sheikh Ponda, waliojikusanya nje ya uzio wa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Alhamisi Novemba 1, 2012

 

 

 

 

 Picha na habari zote na khalfansaid.blogspot.com

KAKA ANG'ARA NA KUFUNGA BAO WAKATI REAL MADRID IKISHINDA 4-1 DHIDI YA ALCOYANO



MADRID, Hispania
REAL Madrid ni kama imeshajihakikishia kucheza hatua ya robo fainali ya Kombe la Mfalme baada ya kushinda ugenini 4-1 dhidi ya Alcoyano huku kiungo wake wa kimataifa wa Brazil, Kaka akionyesha kiwango cha juu na kufunga bao moja usiku wa kuamkia leo.

Karim Benzema alifunga goli la utangulizi na Kaká akaongeza la pili kabla ya mapumziko. Yosso José Rodríguez alifunga la tatu na Benzema akaongeza jingine wakati wenyeji wakipata bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Javi Lara.

Katika mechi hiyo, Real walichezesha yosso wengi katika kikosi kilichoanza ambao ni pamoja na Nacho Fernández, Álex Fernández na Álvaro Morata.