CRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI MPYA 'EL CLASICO' KATI YA REAL MADRID NA BARCELONA
MADRID, Hispania 
Cristiano Ronaldo 
ametokea kuwa na 'mzuka' wa kupachika mabao kila mara anapocheza dhidi 
ya Barcelona na amethibitisha hilo kwa mara nyingine jana usiku pale 
alipofunga mabao yote mawili ya Real Madrid wakati wakitoka sare ya 2-2 
dhidi ya Barca katika 'el clasico' yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.
Kutokana
 na mabao aliyofunga jana  kwenye Uwanja wa Camp Nou, Ronaldo ameandika 
rekodi kwa kuwa mchezaji wa kwanza katika historia kuwahi kufunga katika
 mechi sita mfululizo za 'el clasico' ya mahasimu wa jadi, Barcelona na 
Real Madrid.
Ronaldo alianza kasi yake katika robo fainali ya 
Kombe la Mfalme msimu uliopita, akifunga katika mechi ya kwanza kwenye 
Uwanja wa Santiago Bernabeu na ya marudiano kwenye Uwanja wa Camp Nou.
Aliendeleza
 makali yake katika mechi ya marudiano ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania 
iliyochezwa April 21 wakati alipofunga goli lililowapa Real Madrid 
ushindi wa 2-1 na kuwasafishia njia ya kutwaa ubingwa msimu uliopita wa 
2011/2012.
Wakati walipokutana katika mechi mbili za kuwania taji
 la Super Cup mwanzoni mwa msimu huu, Cristiano pia alifunga katika 
mechi zote na kuisaidia Real kutwaa taji hilo kabla ya jana kufunga tena
 mabao yote mawili ya Real Madrid.
 
 
 
          
      
 
  
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment