Sunday, October 7, 2012

JOSE MOURINHO: BALOTELLI NI KAMA KICHAA...NAWEZA KUTOA KITABU CHA KURASA 200 KUELEZEA VITUKO VYAKE NILIPOKUWA KOCHA WAKE INTERMILAN













MADRID, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amezungumzia kipindi chake cha kuwa na straika Mario Balotelli wa Manchester City wakati akiifundisha Inter Milan na kusema kwamba mchezaji huyo ni kichaa.

Mourinho ameongeza kuwa akitaka, anaweza kuandaa kitabu kitakachoongoza kwa mauzo kuhusiana na migongano yake na Balotelli.

“Naweza kaundika kitabu cha kurasa 200 kuelezea mikwaruzano yangu na Mario wakati wa kipindi changu cha miaka miwili nikiwa na Inter Milan, lakini kitabu chenyewe hakitakuwa cha simulizi – kitakuwa ni cha vidhekesho,” amesema Mourinho.

“Nakumbuka kipindi fulani tulipokwenda kucheza dhidi ya Kazan katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Katika mechi hiyo mastraika wangu wote walikuwa majeruhi. Sikuwa na Diego Milito, wala Samuel Eto’o, nilikuwa na wakati mgumu hasa na Mario ndiye aliyekuwa mchezaji pekee wa nafasi hiyo.

“Mario akapata kadi ya njano katika dakika ya 42, kwa hiyo wakati tulipokuwa kwenye chumba cha kuvalia katika kipindi cha mapumziko nilitumia takriban dakika 14 kati ya 15 zilizopo kuzungumza na Mario tu.

“Nilimwambia: ‘Mario, siwezi kukutoa, sina mastraika wengine katika benchi, kwahiyo usimguse mtu na badala yake cheza mpira tu. Tukipoteza mpira, we usifanye lolote. Kama mtu akikuchokoza, we tulia, kama refa akikosea, we achia tu.'

No comments:

Post a Comment