OLYMPIC LYON WALIPEWA RONALDO KWA BEI SAWA NA BURE WAKAMKATAA
OLYMPIQUE Lyon ingeweza kumsajili nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa bei sawa na bure, imebainika. 
Kocha wa wakati huo wa Sporting Lisbon, 
Laszlo Boloni alitaka kumsajili Tony Vairelles kutoka Lyon kwa 
kubadilishana na wachezaji wawili akiwamo Ronaldo. 
"Sporting de Portugal hawakuwa na pesa 
hivyo walipendekeza kubadilishana wachezaji na walikuwa tayari kuwatoa 
wachezaji wawili, mmoja wao akiwa ni Cristiano Ronaldo, lakini Olympique
 walikataa ...," alibainisha Boloni. 
Muda mfupi baadaye Ronaldo akasajiliwa na Manchester United na yaliyobaki yakawa historia. 

No comments:
Post a Comment