Wednesday, October 24, 2012

MKENYA ANAYECHEZEA CELTIC AISIMAMISHA BARCELONA
Victor Wanyama wa Celtic akishangilia baada ya kufunga goli la pili dhidi ya Helsingborgs IF wakati wa mechi ya kuwania kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Celtic

Wanyama akipongezwa na wachezaji wenzake





























SCOTLAND
Straika wa zamani wa Celtic, John Hartson anaamini kwamba kiungo wa kimataifa wa Kenya, Victor Wanyama ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kumzima 'jini' Lionel Messi wakati watakaposhuka dimbani leo kucheza dhidi ya Barcelona katika mechi ya Kundi G la Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwenye Uwanja wa Nou Camp.

Hartson anaamini kwamba Wanyama ambaye ni ndugu yake Mkenya mwingine, McDonald Mariga, ni kiungo mzuri na anaweza kumzuia Messi kama ilivyokuwa enzi zake mwaka 2004 wakati walipocheza dhidi ya Barca na kupata sare ya 1-1 baada ya kumdhibiti vyema Mbrazil Ronaldinho aliyekuwa ndiye Messi wa wakati huo.

“Ni kazi ngumu sana kumchunga mchezaji mmoja wakati mnapocheza dhidi ya timu kali kama ya Barca, lakini wakati tukienda pale, kulikuwa na Ronaldinho ambaye ndiye aliyekuwa Mwanasoka Bora Na. No duniani,” amesema Hartson.

“Alikuwa ndiye Messi wa wakati huo na Martin O’Neill alimpa majukumu Joos Valgaeren kumchunga wakati wote.

“Joos alikuwa akikimbia naye kila anakokwenda kama suti mwilini na Ronaldinho hakupata nafasi ya kupiga shuti.

“Mnaweza kufanya hivyo pia dhidi ya Messi? Mngeulizwa swali hilo pia wakati wa enzi za Ronaldinho, lakini mbinu hiyo ilitusaidia. Nadhani Wanyama anaiweza kazi hii.

“Sijui ni kitu gani atakachokifanya Lenny. Nadhani atatumia mtindo wa 4-5-1 huku Wanyama akikaa mbele ya beki namba nne kwa ajili ya kusaidia ulinzi.

“Wanyama ana umbo kubwa, ana nguvu, anaweza kunyang'anya mipira na kukimbia nayo. Ni mchezaji mwenye nguvu sana na pia anacheza kwa ushirikiano. Ni mkimbiaji mzuri pia na anacheza kwa kiwango cha juu.”

Monday, October 22, 2012

LIONEL MESSI APIGA HAT-TRICK MARA 19, MAGOLI MANNE @ MECHI MARA 3, MABAO MATANO @ MECHI MARA 1
LIONEL Messi, ambaye alikuwa shujaa wa mechi ya ugenini ya Barcelona dhidi ya Deportivo kwenye Uwanja wa Riazor, amefunga magoli matatu au zaidi mara 23 katika maisha yake ya soka, huku 21 kati ya hizo akiwa na Barcelona na mara mbili akiwa na timu yake ya taifa ya Argentina.

Katika mechi hizo 23, amefunga 'hat-trick' mara 19. Katika mechi tatu kati ya nne zilizobaki alipiku rekodi zake mwenyewe kwa kufunga magoli manne dhidi ya Arsenal, Valencia na Espanyol na katika mechi nyingine moja 'akajifunika' kabisa mwenyewe kwa kufunga magoli matano dhidi ya Bayer Leverkusen mwaka huu katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Akizungumzia ushindi wa timu yake wa 5-4 dhidi ya Deportivo ambapo yeye alifunga 'hat trick', Messi alisema: "Tumeshinda. Daima inakuwa ngumu sana kucheza mechi tukitokea kuziwakilisha timu zetu za taifa, kwasababu unarejea ukiwa umechoka. Huu ulikuwa ni ushindi muhimu," alisema.

'Supastaa' huyo wa Argentina alisema kutokea uwanjani hakuona kama Deportivo walistahili penalti wala kutolewa kwa kadi nyekundu kwa Mascherano. "Sikuona jambo lile. niliambiwa kwamba haikutahili kuwa penalti wala kadi nyekundu, lakini hivyo ndivyo ilivyotokea na refa akaona kinyume," alisema.

Aidha, Messi alipuuza 'hat-trick' aliyofunga pamoja na magoli 59 aliyofunga katika mwaka 2012, ambayo ni rekodi kwa mchezaji wa Barcelona. Katika mwaka huu wa kalenda kuanzia Januari 2012 hadi sasa, Messi ameifungia klabu yake magoli 59 na ameifungia timu yake ya taifa ya Argentina magoli 12 na kufanya jumla ya mabao 71, manne tu pungufu ya rekodi ya wakati wote inayoshikiliwa na Pele aliyefunga magoli 75 mwaka 1959. Messi anatarajiwa kuivunja rekodi hiyo na kuweka yake ya hatari zaidi kwani bado ana zaidi ya miezi miwili ili mwaka huu 2012 umalizike Desemba 31.

"Tunachopaswa kufanya ni kuendelea kushinda, kucheza katika kiwango tulichokuwa nacho kabla ya mapumziko ya kwenda kuzitumikia timu zetu za taifa. Takwimu za 'hat-trick' si muhimu, kushinda mechi zetu ndiyo muhimu, pamoja na kuchangia mafanikio ya klabu," alisema.

Saturday, October 20, 2012

SHAMBA LA MCHUNGAJI MWINGIRA LACHOMWA MOTO
Shamba la Malonje linalomilikiwa na Kanisa la Efatha limepata hasara kubwa baada ya wananchi wa kijiji cha Sikaungu wilayani Sumbawanga vijijini mkoani Rukwa, kujichukulia sheria mkononi na kuvamia moja ya kambi ya Shamba hilo iitwayo Sikaungu na kuyateketeza kabisa matrekta mawili makubwa aina ya New Holland na kubomoa baadhi ya nyumba kwenye kambi hiyo. Mchungaji Kiongozi Michael Meela wa Kanisa la Efatha mkoani Rukwa akiongelea kuhusu suala hilo alisema hasara iliyopatikana ni zaidi ya shilingi milioni 228 na kwamba tukio hilo lilitokea mara tu baada ya Mbunge wa Jimbo la Kwela Mh. Ignas Malocha kuhutubia mkutano wa hadahara kijijini hapo na kuwahamasisha wananchi watumie nguvu ya umma kuyakomboa mashamba yao yaliyochukuliwa na mwekezaji huyo.Kamanda wa polisi wa mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwaruanda akithibitisha kuhusu sakata hilo alisema tayari wanawashikilia watu 11 kwa tuhuma za kufanya uharibifu huo mkubwa namsako unaendelea kuwatafuta wengine waliohusika katika tukio hilo.

Friday, October 12, 2012

OLYMPIC LYON WALIPEWA RONALDO KWA BEI SAWA NA BURE WAKAMKATAA


OLYMPIQUE Lyon ingeweza kumsajili nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo kwa bei sawa na bure, imebainika. 

Kocha wa wakati huo wa Sporting Lisbon, Laszlo Boloni alitaka kumsajili Tony Vairelles kutoka Lyon kwa kubadilishana na wachezaji wawili akiwamo Ronaldo. 


"Sporting de Portugal hawakuwa na pesa hivyo walipendekeza kubadilishana wachezaji na walikuwa tayari kuwatoa wachezaji wawili, mmoja wao akiwa ni Cristiano Ronaldo, lakini Olympique walikataa ...," alibainisha Boloni. 


Muda mfupi baadaye Ronaldo akasajiliwa na Manchester United na yaliyobaki yakawa historia.

Wednesday, October 10, 2012


CRISTIANO RONALDO ANUNUA GARI YA SHILINGI MIL 415

MADRID, Hispania
NYOTA wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amejawa na furaha tele kutokana na kiwango cha juu alichoanza nacho msimu huu na kuamua kujipongeza kwa kujinunulia gari dogo jipya la kifahari kwa ajili ya kutanulia mitaani.

Gazeti la Marca limeandika leo kuwa Ronaldo amenunua gari hilo jipya aina ya McLaren MP4-12C Spyder kwa dola za Marekani 268,000 (Sh. milioni 415).

Sifa mojawapo kubwa ya gari hilo la kisasa ni kasi yake ya kuchanganya mwendo kwani linapowashwa tu, huwa na uwezo wa kufikia spidi ya kilomita 100 kwa saa baada ya muda mfupi wa sekunde 3.1.

Ronaldo alionekana juzi katika maeneo ya kwao, Lisbon nchini Ureno ambako amekwenda kuungana na wenzake katika kambi ya kikosi cha timu ya taifa ya Ureno.  

Mbali na gari hilo jipya (McLaren MP4-12C Spyder) Ronaldo pia anamiliki magari kadhaa ya kifahari likiwamo aina ya Lamborghini Aventador LP700-4.
MLINZI WA LIONEL MESSI ATOA KALI YA MWAKA
Kutoka kulia ni baunsa wa zamani wa Lionel Messi, Daniel Rojo, Messi mwenyewe, muimbaji wa Argentina Andrés Calamaro na Javier Mascherano wakifurahi wakati wakipozi kwa picha ya pamoja.

Daniel Rojo akiwa katika maeneo ya Barcelona
BARCELONA, Hispania
Barcelona waliwahi kuajiri bodigadi wa kumlinda Lionel Messi aliyekuwa na rekodi ya kutisha ya kuwahi kufanya uporaji katika benki MIA TANO!

Baunsa huyo aitwaye Daniel Rojo amezungumzia maisha yake katika kipindi chote cha kumlinda Messi na kufichua mengi kuhusiana na maisha yake wakati akihojiwa na Gazzetta dello Sport.

"Katika maisha yangu nimewahi kufanya uporaji kwenye benki 500. Nilipenda sana maisha ya juu, magari na nguo za bei mbaya, na dawa za kulevya. Nilianza wakati nikiwa na miaka 15 na baadaye nikawa mtaalam," alifichua Rojo.

“Mwaka 1997 niliamua kubadili maisha yangu na kujiunga na dunia ya soka. Mwaka 2006 nilianza kufanya kazi Barcelona. Wakati huo, (Frank) Rijkaard alikuwa ndiye kocha na timu ilinituma kuwafuata wachezaji waliokuwa wakilewa sana katika klabu za usiku na kushindwa kuendesha.”

Kuhusu Messi, Rojo aliendelea: “Siku moja walinituma kumfuata baada ya mazoezi. Messi ni mtoto mpole na wakati akila alikuwa akikaa kando yangu huku mimi nikimsimulia maisha yangu. Hakuwa na mengi ya kusema, katika maisha yake hakuwa akifanya jambo jingine lolote mbali na mazoezi na kucheza soka. Hawakumruhusu pia kwenda kujirusha na wasichana, ni hivi sasa tu ndipo amejua maisha yanamaanisha nini."

Aliendelea: “Sijafanya nao kazi kwa miaka kadhaa sasa lakini mara moja moja huwa tunakutana njiani. Mwaka uliopita nilikwenda kuangalia mechi ya Barcelona na rafiki zangu na kukutana na Leo aliyekuwa ameambatana na akina dada wawili warembo sana. Baadaye, nilitambua kwamba mmoja alikuwa mpenzi wake, Antonella Roccuzzo, na mwingine alikuwa ni mke wa (Javier) Mascherano na tukatoka wote kwenda kula. Mwishoni, Leo alinirudisha nyumbani kwangu huku nikiwa nimeketi kiti cha nyuma."
CRISTIANO RONALDO AZIDI KUFUATILIA REKODI YA RAUL REAL MADRID

MADRID, Hispania
KWENYE Uwanja wa Nou Camp, Cristiano Ronaldo alifunga goli lake la 160 na la 161 la mechi za kimashindano akiwa na jezi ya Real Madrid.

Raul alitumia misimu 16 kufikisha magoli 323, ambayo ndiyo rekodi ya wakati wote ya klabu hiyo, wakati Ronaldo tayari amefikisha nusu (49.8%) kwa misimu mitatu tu.

Cristiano hivi sasa anashika nafasi ya tisa katika orodha ya wafchezaji waliofunga magoli mengi zaidi katika historia ya Real Madrid, akiwa amempita Amancio Amaro – ambaye alifunga magoli 155 katika misimu 14 – katika mechi dhidi ya Deportivo.

Hata hivyo, ni wastani wa kufunga magoli mengi ndio unaomfanya Ronaldo abaki kuwa wa kipekee: katika misimu mitatu kamili kufikia sasa akiwa na klabu hiyo, amefunga wastani wa magoli 48.6 kwa msimu. Kwa maneno mengine, wakati Raul alihitaji kucheza mechi 741 ili kuweka rekodi hiyo, Ronaldo amefikia nusu yake kwa kucheza mechi 155 tu.

Kama Ronaldo ataendelea na kasi yake na kumaliza miaka mitatu iliyobaki kati ya sita ya mkataba wake wa sasa, inamaanisha kuwa atafikisha jumla ya magoli 292, ambayo yatakuwa ni magoli 31 pungufu ya rekodi ya Raul – pengo ambalo ni dogo kwa mtu ambaye alifunga magoli 54 katika msimu wa 2010-11 na magoli 60 katika msimu 2011-12 katika michuano yote.

Kati ya wachezaji nane walio mbele ya CR7 katika orodha ya wafungaji bora wa wakati wote Madrid (Butragueno na Pirri, ambao wamelingana katika magoli 171, ndio wanaotarajiwa kufuatia kupitwa na mshambuliaji huyo mzaliwa wa Madeira, Ureno), huku Ferenc Puskas (mwenye wastani wa goli 0.92 kwa mechi) ndiye pekee mwenye wastani mzuri zaidi ya Ronaldo katika kufumania nyavu.

STAILI YA UNYOAJI NYWELE YA RONALDO YAWEKWA WAZI NA KINYOZI WAKE
 

Vinyozi wa Cristiano Ronaldo, Jose Miguel na Siero Leal

CRISTIANO Ronaldo alimshangaza kila mmoja kwenye Uwanja wa Nou Camp Jumapili kutokana na mwonekano mpya. Ilikuwa ni staili ya nywele iliyoonyesha alama ya V. Wakati alipofunga goli la kwanza alionyesha kidole chake kwenye alama ya ushindi kichwani mwake. Kuna stori nyuma ya staili hiyo.

Mreno huyo aliwapa vinyozi ambao ni ndugu Jose Miguel na Siero Leal. Aliwaita Jumamosi na kuwaeleza kwamba anatafuta staili mpya, kitu tofauti na kitakachozua mjadala.

"Alituambia, kama ilivyo mara nyingi kwake, anahitaji kitu tofauti. Tunamfahamu vyema na tukapata wazo la kumnyoa kwa alama ambayo inamaanisha amani na utulivu ambao huupata shujaa baada ya mapambano. Alikubali," alisema mmoja wa vinyozi hao.

Kuifanya ionekane kitu kizuri ilikuwa ni jambo jepesi. Jose alisema: "Sio tu staili. Kuna sababu katika kila staili ya kunyoa. Na anahitaji staili inayoonekana. Inamfaa. Yeye ni mwenye malengo na anayependa vitu bora. Tulifanya alimbunia kilichokuwa katika hisia zake kwa wakati ule na kilionekana wakati wa mechi".

"Nywele zake ni laini sana na unapaswa kuzinyoa kwa umakini. Anapenda kuziseti ama kuzipaka mafuta mengi. Anafahamu kwamba kamera za televisheni humfuatilia kwa kila afanyalo na anapenda kuonekana mtanashati. Cristiano anajioenda sana na anapenda kutimiza malengo. Ni mshindi. Anajifikiria yeye tu," aliongeza.
J-LO KUMBE NI SHABIKI MKUBWA SANA WA REAL MADRID





Monday, October 8, 2012

MOURINHO: KUMLINGANISHA RONALDO NA MESSI SASA NI MARUFUKU

















KOCHA wa Real Madrid, Jose Mourinho amewasifu Cristiano Ronaldo na nyota wa Barcelona, Lionel Messi baada ya wawili hao kufunga mara mbili kila mmoja katika sare ya 2-2 juzi usiku na ametaka ipigwe marufuku kuwalinganisha. 

Alipoulizwa nani anapaswa kutwaa tuzo ya Ballon d'Or ya mwanasoka bora wa dunia, alisema: "Sitaki kuiwaza sana hiyo. 

"Nadhani ipigwe marufuku sasa kusema nani ni mwanasoka bora wa dunia kwa sababu hawa wawili ni wa sayari nyingine. 

"Ningependa mchezaji wangu ashinde kwa sababu yeye ni bingwa wa ligi bora duniani, lakini nadhani wote ni wachezaji wazuri sana."
CRISTIANO RONALDO AWEKA REKODI MPYA 'EL CLASICO' KATI YA REAL MADRID NA BARCELONA



MADRID, Hispania 

Cristiano Ronaldo ametokea kuwa na 'mzuka' wa kupachika mabao kila mara anapocheza dhidi ya Barcelona na amethibitisha hilo kwa mara nyingine jana usiku pale alipofunga mabao yote mawili ya Real Madrid wakati wakitoka sare ya 2-2 dhidi ya Barca katika 'el clasico' yao ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania.

Kutokana na mabao aliyofunga jana  kwenye Uwanja wa Camp Nou, Ronaldo ameandika rekodi kwa kuwa mchezaji wa kwanza katika historia kuwahi kufunga katika mechi sita mfululizo za 'el clasico' ya mahasimu wa jadi, Barcelona na Real Madrid.

Ronaldo alianza kasi yake katika robo fainali ya Kombe la Mfalme msimu uliopita, akifunga katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu na ya marudiano kwenye Uwanja wa Camp Nou.

Aliendeleza makali yake katika mechi ya marudiano ya La Liga, Ligi Kuu ya Hispania iliyochezwa April 21 wakati alipofunga goli lililowapa Real Madrid ushindi wa 2-1 na kuwasafishia njia ya kutwaa ubingwa msimu uliopita wa 2011/2012.

Wakati walipokutana katika mechi mbili za kuwania taji la Super Cup mwanzoni mwa msimu huu, Cristiano pia alifunga katika mechi zote na kuisaidia Real kutwaa taji hilo kabla ya jana kufunga tena mabao yote mawili ya Real Madrid.

Sunday, October 7, 2012

JOSE MOURINHO: BALOTELLI NI KAMA KICHAA...NAWEZA KUTOA KITABU CHA KURASA 200 KUELEZEA VITUKO VYAKE NILIPOKUWA KOCHA WAKE INTERMILAN













MADRID, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amezungumzia kipindi chake cha kuwa na straika Mario Balotelli wa Manchester City wakati akiifundisha Inter Milan na kusema kwamba mchezaji huyo ni kichaa.

Mourinho ameongeza kuwa akitaka, anaweza kuandaa kitabu kitakachoongoza kwa mauzo kuhusiana na migongano yake na Balotelli.

“Naweza kaundika kitabu cha kurasa 200 kuelezea mikwaruzano yangu na Mario wakati wa kipindi changu cha miaka miwili nikiwa na Inter Milan, lakini kitabu chenyewe hakitakuwa cha simulizi – kitakuwa ni cha vidhekesho,” amesema Mourinho.

“Nakumbuka kipindi fulani tulipokwenda kucheza dhidi ya Kazan katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya. Katika mechi hiyo mastraika wangu wote walikuwa majeruhi. Sikuwa na Diego Milito, wala Samuel Eto’o, nilikuwa na wakati mgumu hasa na Mario ndiye aliyekuwa mchezaji pekee wa nafasi hiyo.

“Mario akapata kadi ya njano katika dakika ya 42, kwa hiyo wakati tulipokuwa kwenye chumba cha kuvalia katika kipindi cha mapumziko nilitumia takriban dakika 14 kati ya 15 zilizopo kuzungumza na Mario tu.

“Nilimwambia: ‘Mario, siwezi kukutoa, sina mastraika wengine katika benchi, kwahiyo usimguse mtu na badala yake cheza mpira tu. Tukipoteza mpira, we usifanye lolote. Kama mtu akikuchokoza, we tulia, kama refa akikosea, we achia tu.'

MAJINA YA WANOWANIA TUZO ZA MCHEZAJI BORA AFRICA HAWA HAPA!!!

CAIRO, Misri
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limetaja majina ya awali ya wachezaji nyota 34 barani wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika Mwaka 2012 ambamo ndani yake, wamejaa 'maproo' 29 wanaocheza soka la kulipwa nje ya Afrika huku nyota wa TP Mazembe, Mtanzania Mbwana Samatta na Tressor Mputu wanaong'ara katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika wakikosekana kwenye orodha hiyo.

Miongoni mwa wanaocheza soka la kulipwa Ulaya ni mshindi wa tuzo hiyo msimu uliopita, kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Manchester City ya England, Yaya Toure, mastraika nyota wa Newcastle United -- Papiss Demba Cisse na Demba Ba na pia winga wa Arsenal, Gervinho..


Wachezaji watatu wanaocheza katika klabu za Afrika ni Wazambia Rainford Kalaba na Stoppila Sunzu wanaoichezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Youssef Msakni wa Esperance ya Tunisia.


OROTHA KAMILI:

1.    Abdelaziz Barrada - Getafe (Hispania) na Morocco

2.    Adel Taarabt - Queens Park Rangers (England) na Morocco

3.    Alain Sibiri Traore - Lorient (Ufaransa) na Burkina Faso

4.    Alexander Song - Barcelona (Hispania) na Cameroon

5.    Andre 'Dede' Ayew - Marseille (Ufaransa) na Ghana

6.    Arouna Kone - Wigan (England) na Ivory Coast

7.    Aymen Abdennour - Toulouse (Ufaransa) na Tunisia

8.    Bakaye Traore - AC Milan (Italia) na Mali

9.    Cheick Tiote - Newcastle United (England) na Ivory Coast

10.    Christopher Katongo - Henan Construction (China) na Zambia

11.    Demba Ba - Newcastle United (England) na Senegal

12.    Didier Drogba - Shanghai Shenhua (China) na Ivory Coast

13.    Emmanuel Agyemang-Badu - Udinese (Italia) na Ghana

14.    Emmanuel Mayuka - Southampton (England) na Zambia

15.    Foxi Kethevoama - FC Astana (Kazakhstan) na Afrika ya Kati.

16.    Gervinho - Arsenal (England) na Ivory Coast

17.    Hilaire Momi - Le Mans (Ufaransa) na Afrika ya Kati.

18.    John Obi Mikel - Chelsea (England) na Nigeria

19.    John Utaka - Montpellier (Ufaransa) na Nigeria

20.    Kwadwo Asamoah - Juventus (Italia) na Ghana

21.    Moussa Sow - Fenerbahce (Uturuki) na Senegal

22.    Nicolas N'koulou - Marseille (Ufaransa) na Cameroon

23.    Papiss Demba Cisse - Newcastle United (England) na Senegal

24.    Pape Moussa Konate - FC Krasnodar (Urusi) na Senegal

25.    Pierre-Emerick Aubameyang - St Etienne (Ufaransa) na Gabon

26.    Rainford Kalaba - TP Mazembe (DR Congo) na Zambia

27.    Seydou Doumbia - CSKA Moscow (Urusi) na Ivory Coast

28.    Seydou Keita - Dalian Aerbin (China) na Mali

29.    Sofiane Feghouli - Valencia (Hispania) na Algeria

30.    Stoppila Sunzu - TP Mazembe (DR Congo) na Zambia

31.    Victor Moses - Chelsea (England) na Nigeria

32.    Yaya Toure - Manchester City (England) na Ivory Coast

33.    Younes Belhanda - Montpellier (Ufaransa) na Morocco

34.    Youssef Msakni - Esperance (Tunisia) na Tunisia

Saturday, October 6, 2012

MAAJABU YA MAGOLI ANAYOFUNGA AARON RAMSEY WA ARSENAL
Kila mara mchezaji wa Arsenal Aaron Ramsey anapofunga goli, mtu maarufu anakufa siku inayofuata.

May 1, 2011 = Ramsey alifunga bao dhidi ya Man Utd.
OSAMA BIN LADEN akafa siku inayofuata

Oct 2, 2011 = Ramsey alifunga dhidi Spurs
STEVE JOBS muasisi na mmiliki wa kampuni ya Apple akafa siku iliyofuata.

Oct 19, 2011 = Ramsey akafunga dhidi ya Olympic Marsellie
MUNMMAR GADDAFI akafa siku iliyofauta.

Feb 11, 2012 = Ramsey akatia kambani dhidi Sunderland
WHITNEY HOUSTON akafariki siku iliyofuata.


Aug 4, 2012 = Ramsey akafunga dhidi ya South Korea
KIRK URSO akavuta siku ya pili yake.

Oct 3, 2012(Jana) = Ramsey alifunga dhidi ya Olympiakios
Waziri mkuu wa Syria amethibitishwa kuaga dunia leo hii.
MOURINHO: NINA FURAHA SANA HAPA REAL MADRID......SIONDOKI MPAKA MKATABA WANGU UMALIZIKE HAPO 2014





















MADRID, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema kuwa ana furaha tele katika klabu yake inayoshikilia ubingwa wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania na kwamba hafikirii kuondoka kabla ya kumalizia mkataba mwingine mpya aliosaini hivi karibuni wa kubaki klabuni hapo kwa miaka minne zaidi.

Mourinho ametoa ufafanuzi huo kufuatia uvumi uliotanda kwamba yuko mbioni kurudi kufundisha katika klabu za Ligi Kuu ya England.

“Nina furaha na ninataka kubaki hapa. Nimesaini mkataba mwingine na Real Madrid utakaonibakiza kwa miaka mingine minne, ni kwa sababu sisi ni klabu bora zaidi duniani.

“Kufuatia mataji niliyotwaa England na Italia, Real Madrid ilikuwa inakosekana katika CV yangu. Na sasa kwa sababu tayari ninayo, ninapaswa kufanya kazi kwa uwezo wangu wote.

“Hata hivyo nilikuwa na furaha sana jijini London, na nitarudi tu.”
PICHA ZAIDI ZA RICK ROSS The Big Boss ALIPOWASILI BONGO
Meneja wa Bia ya Serengeti ambao ndio wadhamini wakuu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012,Allan Chonjo akisalimiana na Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Rick Ross mara baada ya kuwasili usiku huu ndani ya uwanija wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,akiwa na baadhi ya wanamuziki wenzake pichani nyuma,kati ni Oparesheni Meneja wa Prime Time Promotions Ltd,Balozi Kindamba ambao ndio waratibu wa tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linalotarajiwa kufanyika hapo leo.






















Rick Ross akitoa salamu ya salut kwa washabiki wake waliojitokeza usiku huu (hawapo pichani) kumlaki


























Operesheni Meneja wa Prime Time Promotions,Balozi Kindamba akiwaongoza wageni wake kuelekea kwenye gari tayari kuondoka kuolekea kwenye hoteli waliopangiwa kufikia usiku huu,Shoto ni Rick Ross na akiwa na baadhi wanamuziki wenzake aliombatana nao .




































Rick Ross akiingia ndani ya gari tayari kuanza safari ya kuelekea hotelini

Rick Ross akiondoka na mchuma wake kuelekea hotelini

Friday, October 5, 2012

HIZI NDIZO PICHA ZA RICK ROSS ALIPOWASILI BONGO JANA USIKU!!!