Sheikh Ponda Issa Ponda, akifunguliwa
pingu, baada ya kufikishwa kwenye chumba cha mahakama ya hakimu mkazi
Kisutu jijini Dar es Salaam jana Alhamisi Novemba 1, 2012. Kiongozi huyo
mwenye msimamo mkali, alifikishwa kwa mara ya pili jana pamoja na
wafuasi wake ambapo hakimu anayesikiliza kesi dhidi yake, Victoria
Nongwa, ya kuvamia eneo la Markaz, Chang'ombe jijini Dar es Salaam,
ambapo waliharibu na kuiba mali vyote vikiwa na thamani ya shilingi
milioni 59, madai ambayo washtakiwa wote waliyakanusha. Hakimu huyo
alikubali kutoa dhamana kwa washtakiwa wote isipokuwa kiongozi huyo
ambaye ni mshtakiwa namba 1 kwa madai kuwa bado Mkurugenzi was Mashtaka
nchini (DPP), hajaondoa pingamizi lake la kuzuia dhamana kwa mshtakiwa
namba moja. Ulinzi katika mahakama hiyo haujawahi kutokea katika miaka
ya hivi karibuni, ambapo pamoja na mambo mengine, palifungwa CCTV
Cameras, vifaa vya kugundua vitu vyenye asili ya chuma, polisi wa
kutuliza gharsia magereza na wale wa FFU, polisi wa farasi na mbwa,
pamoja na askari kanzu waliotapakaa kila kona ya maeneo jirani na
mahakama hiyo kubwa jijini Dar es Salaam. Kikundi kidogo cha wafuasi wa
ssheikh Ponda, kilijaribu kuleta rabsha, lakini polisi walitumia busara
na kuwaelekeza kilichoamuliwa mahakamani ambapo pamoja na kusuasua
kuondoka eneo hilo la mahakama, lakini hatimaye waliondoka huku polisi
wa kutuliza ghasia wakiwafuata kwa nyuma hadi eneo la makutano ya
barabara za Bibi Titi na ile ya Morogoro nao wakatawanyika. Kwa mujibu
wa vyanzo vya uhakika vya habari, kulikuwepo taarifa kuwa wafuasi hao
walipanga kutega milipuko kwenye eneo la mahakama na pia walisambaza
vipeperushi vyenye vitisho kadhaa, ikiwa ni pamoja na kufanbya
maandamano makubwa ya kulazimisha kiongozi huyo aachiliwe. Kesi hiyo
iliahirishwa hadi Novemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena |
No comments:
Post a Comment